(Eeh baba, twende)
Mungu yu mwema, rehema zake ni za milele
(Haleluya, msifuni)
Hata kama ulishamwasi Mungu
Ukitubu leo, yeye atakusamehe
Hata kama umeua watu wengi
Umehukumu wasio na hatia moyoni
Umekuwa mzizi, mlevi, tena mwizi
Bado Mungu anasema njoo, atakusamehe
Umekuwa mchawi, umeroga watu
Umetenda machukuzo, tubu urejee
Mungu anasamehe, yeye ni wa rehema
Anasamehe, anasahau dhambi zote
Malaika wanangoja, waishangilie toba
Rudi kwake, rudi kwa Baba
Yawezekana wewe kiongozi wa Taifa
Katika mikono yako wengi wameonewa
Wameteswa, wameumizwa, wengine kupotea
Pengine moyo wako unauma kwa maumivu
Unanyooshewa vidole kwa sababu ya kiti
Usijikatae mbele za Mungu leo
Jiachilie kwake, yeye anakupenda
Mungu anasamehe, yeye ni wa rehema
Anasamehe, anasahau dhambi zote
Malaika wanangoja, waishangilie toba
Rudi kwake, rudi kwa Baba
Pengine wewe ni kichwa cha familia
Umekuwa kinyume na wajibu wako
Mungu anakuita, rudi kwenye njia
Ufunguliwe siri ya neema yake
(Praise God, asante Yesu!)
Ona mwanga unakuja sasa hivi
Usikubali giza likutawale tena
Toba yako ni funguo ya baraka
Chukua hatua, Mungu anakusubiri
Mungu anasamehe, yeye ni wa rehema
Anasamehe, anasahau dhambi zote
Malaika wanangoja, waishangilie toba
Rudi kwake, rudi kwa Baba
Rudi kwake, yeye anakupenda
Mungu anasamehe (Haleluya!)
Eeh Baba, tunasifu jina lako
(Safi, twende mbinguni)