(Sawa sawa, sikilizeni baba yenu)
Ahsante Mungu, twende!
Watoto wangu Grey Senga, msikilize
Kwanza tumshukuru Mungu kwa uzima na afya njema
Sema ahsante Mungu, sema tena
Alitupa ridhiki, akatupa pumzi ya uhai
Tumewalea kwa mapenzi, mpaka sasa mmekua
Wengine wana familia, wengine wanajenga maisha
Safari ni ndefu lakini Mungu ni mwema
Pendaneni watoto wangu, shirikianeni
Umoja ni nguvu, upendo ndio msingi wa kila kitu
Wakubwa pendeni wadogo, muwasaidie
Ili nao wakue, wajue kujitegemea
Ahsante Mungu, twendelee hivi
Dunia ya sasa sio ile tuliyokulia sisi
Dunia imebadilika, imejaa changamoto nyingi
Isanga kakondika, macho yanajionea mengi
Lakini nyie msiogope, simameni imara
Muishi pamoja mkimtegemea yeye juu
Sisi wazazi tumechoka, ni zamu yenu kutushika
Kutulea kwa heshima, ndio wajibu wenu sasa
Pendaneni watoto wangu, shirikianeni
Umoja ni nguvu, upendo ndio msingi wa kila kitu
Wakubwa pendeni wadogo, muwasaidie
Ili nao wakue, wajue kujitegemea
Ahsante Mungu, twendelee hivi
Majirani na ndugu wote wapendeni
Msiishi kwa majivuno, unyenyekevu ndio utukufu
Ee Mungu wajaalie uzima wanangu wote
Wapushe na mabalaa, wape afya njema
Kumbukeni nyumbani ni pale upendo ulipo
Kila mmoja akicheka, mimi nafarijika
Grey Senga, jina lenu litasonga mbele
Kwa upendo na imani, tutashinda kila vita
Asambe, twende pamoja, maisha ni safari
Pendaneni watoto wangu, shirikianeni
Umoja ni nguvu, upendo ndio msingi wa kila kitu
Wakubwa pendeni wadogo, muwasaidie
Ili nao wakue, wajue kujitegemea
Ahsante Mungu, twendelee hivi
Pendaneni, shirikianeni
Sawa, mwanangu Grey Senga
Ahsante Mungu kwa yote
(Sho, amani iwe nanyi)
Tunazidi kusonga, sharp sharp