Bongo! Twende!
Atanas Wamunyinyi, kiongozi wetu!
Mheshimiwa Atanas Wafula Wamunyinyi,
Omukimweyi wetu, shujaa wa Kanduyi,
Kama Le Pasteur Lukhendu Nyukuri Omukoyabe,
Ninakupa kongole kwa kazi yako nzuri.
Sasa tunaona mwanga ndani ya giza,
Umejitolea kwa dhati kututetea,
Kanduyi yote inakuamini wewe baba,
2027 tunasonga mbele na wewe.
Atanas Wamunyinyi, kiongozi shupavu,
Kanduyi inakupenda, wewe ni mwanajumuiya,
Wewe ni sauti ya wanyonge wa Bungoma,
Kura ya Kanduyi ni yako, tunajua.
Atanas Wamunyinyi, jembe letu la nguvu,
Tunakuamini wewe, kiongozi hodari.
Ulipigania Nzoia Sugar ilipokuwa taabani,
Bungoma KMTC na shule ya Namachanja,
Zilirudi kwetu kwa sababu ya juhudi zako,
Hukukata tamaa hata kwenye magumu.
Kiwanja cha ndege na hospitali ya rufaa,
Zilizonyakuliwa utazirejesha mikononi mwetu,
Mimi mtoto wa Salome nakutakia mema,
Uongozi wako ni baraka kwa wengi.
Atanas Wamunyinyi, kiongozi shupavu,
Kanduyi inakupenda, wewe ni mwanajumuiya,
Wewe ni sauti ya wanyonge wa Bungoma,
Kura ya Kanduyi ni yako, tunajua.
Atanas Wamunyinyi, jembe letu la nguvu,
Tunakuamini wewe, kiongozi hodari.
Shikana na Wamboka na Majimbo,
Ninyi ndio sauti ya Bungoma yote,
Linda Mwananchi na chama cha TEP,
Edwin Sifuna, rais wetu wa awamu ya sita,
Twende pamoja, umoja ni nguvu yetu,
Atanas baba, endelea kutuongoza.
Sisi sasa ni mayatima kwa uongozi uliopo,
Tunakuhitaji wewe uwe kiongozi wetu,
Mimi kama Le Pasteur naimba sifa zako,
Kazi yako inaonekana, haiwezi kufichika,
Kanduyi inang'ara, matumaini yamerejea,
Tupo nyuma yako, hatutakuacha kamwe.
Atanas Wamunyinyi, kiongozi shupavu,
Kanduyi inakupenda, wewe ni mwanajumuiya,
Wewe ni sauti ya wanyonge wa Bungoma,
Kura ya Kanduyi ni yako, tunajua.
Atanas Wamunyinyi, jembe letu la nguvu,
Tunakuamini wewe, kiongozi hodari.
Asante baba kwa kusimama na sisi,
Atanas Wamunyinyi, kiongozi wa wengi,
Kanduyi ni yako, 2027 twende,
Poa sana, asante sana!
WCB! Tamu!