(Mambo! Bwana Yesu apewe sifa)
(Tunamwimbia yeye aliyetoa damu yake)
(Twende)
Damu imebubujika
Ni ya Immanueli
Wakioga wenye taka
Husafiwa kweli
Naijua nguvu ya msalaba
Inaponipa uzima tele
Ooh damu ya thamani
Inayotuosha dhambini
Twaimba sifa zako Bwana
Sifa zako milele
(Safi! Kali!)
Ilimpa kushukuru
Mwivi mautini
Nami nisiye udhuru
Yanisafi ndani
Kondoo wa kuuawa
Damu ina nguvu
Ooh damu ya thamani
Inayotuosha dhambini
Twaimba sifa zako Bwana
Sifa zako milele
Bwana tangu damu yako
Kunisafi kale
Nimeimba sifa zako
Sitaacha milele
(Twende! Eeh Baba!)
Nikifa tazidi kwimba
Sifa za wokovu
Ulimi ujaponyamaa
Vumbini mwa ufu
Bwana umenikirimu
Nisiyestahili
Ooh damu ya thamani
Inayotuosha dhambini
Twaimba sifa zako Bwana
Sifa zako milele
Nikubali kukwimbia
Mbinguni milele
Mungu nitakusifia
Jina lako pweke
(Asante Yesu, eeh Baba!)
(Tunaabudu, milele)