Bongo! Twende!
Leo tunasherehekea kiongozi shupavu, Bakoki Jack Wanami Wamboka!
Mimi kama Le Pasteur Lukhendu Nyukuri, mtoto wa Salome,
Leo nasimama kidete kukuimbia wewe shujaa,
Bakoki Jack Wanami Wamboka, omuyaya wetu,
Kiongozi wa ukweli, mtetezi wa wanyonge wa Bumula,
Umesimama kidete, ulikataa hongo mbele ya pesa,
Umeamua kutembea na mwananchi wa chini daima.
Bakoki Wamboka, wewe ni simba wa Bumula,
Umeleta mabadiliko, tunaona nuru inang’aa,
Kura ya 2027 ni yako, twende na TEP,
Linda mwananchi, kiongozi asiye na woga,
Bakoki Wamboka, wewe ni mkombozi wetu,
Bumula inasonga mbele, wewe ndiye kiongozi!
Shule zimejengwa kwa mikono yako mitukufu,
Kutoka Kibuke mpaka Kimaeti, tunashuhudia kazi,
Sango, Myanga, Lumboka, mpaka Khasoko, umeacha alama,
Kwa mara ya kwanza dunia inakiri Bumula ina kiongozi,
Umekaa na Majimbo, Wamunyinyi, na Natembeya,
Mnajenga Usawa, TEP ndiyo njia yetu leo.
Bakoki Wamboka, wewe ni simba wa Bumula,
Umeleta mabadiliko, tunaona nuru inang’aa,
Kura ya 2027 ni yako, twende na TEP,
Linda mwananchi, kiongozi asiye na woga,
Bakoki Wamboka, wewe ni mkombozi wetu,
Bumula inasonga mbele, wewe ndiye kiongozi!
Tunamuunga mkono Edwin Watenya Sifuna,
Rais wetu wa awamu ya sita, tunasonga mbele,
Mungu akupe nguvu, amani, na maisha marefu,
Bakoki wewe ni kiongozi wetu wa milele,
Tamu! Poa! Mambo yote ni swafi na wewe.
Umetupigania kwa hali na mali bila kuchoka,
Simba Lundi Emboko, jina lako litadumu sana,
Bumula inajivunia kuwa na kiongozi kama wewe,
2027 kura ni TEP, ushindi ni wetu dhahiri,
Tunakutakia heri, kazi yako inaonekana wazi,
Bumula inashangilia, kiongozi wetu hodari!
Bakoki Wamboka, wewe ni simba wa Bumula,
Umeleta mabadiliko, tunaona nuru inang’aa,
Kura ya 2027 ni yako, twende na TEP,
Linda mwananchi, kiongozi asiye na woga,
Bakoki Wamboka, wewe ni mkombozi wetu,
Bumula inasonga mbele, wewe ndiye kiongozi!
Bakoki Wamboka, shujaa wetu,
Bumula inakuamini, TEP ndiyo habari ya mujini,
Ah ah! Twende kazi, tunasonga mbele,
Maisha marefu kwa kiongozi wetu, Bongo!