MWANGA WA EBUYALU
A klassique media production
Ninatoka Ebuyalu, kijiji cha dhiki,
Ambapo ada imekuwa mwiba wa safari,
Wenzangu waliacha shule, ndoto zikabaki,
Macho yakatazama mbali, mioyo ikalia kimya.
Tulikuwa na ndoto, tukataka kufika mbali,
Lakini mifuko mitupu ikatufunga njia,
Mmoja akaenda huku, mwingine akaenda kule,
Na wengine wakanaswa na moshi wa 'msala.'
Ebuyalu, Ebuyalu, taa yangu yawaka,
Ebuyalu, Ebuyalu, ndoto yangu yazuka!
Nimepata nafasi, sitaiangusha chini,
Kwa elimu na nidhamu, tutainua kijiji!
Msala si dawa, msala ni mtego,
Bangi si rafiki, ni shimo la mwanguko!
Tushike vitabu, tuache moshi wa huzuni,
Ebuyalu yetu kesho itang'aa kwa nuru!
Nikafika Shule ya Upili ya Ebuyalu,
Nikakutana na mlango wa tumaini,
Nikapata ufadhili wa masomo, nikabaki shuleni,
Kalamu yangu ikarudi, nikaanza kuota tena.
Nikashukuru kwa mkono ulioniinua,
Kwa nafasi niliyopewa nisipotee njiani,
Lakini moyoni nina swali linaloniumiza—
Wenzangu waliobaki, nani atawainua?
Mwalimu Mkuu Alfred Amani, nakushukuru,
Kwa kulinda kesho yetu kwa moyo wa mwalimu,
Alfred Amani, wewe ni nguzo ya shule,
Pamoja na walimu, Naibu mwalimu mkuu, walimu wa darasa, walimu wote na wafanyi kazi wa shule, mmetuweka kwenye njia.
Idara ya ushauri nasaha yatufumbua macho,
Yatufundisha madhara ya bangi na msala,
Mnatukumbusha mwili ni hekalu, akili ni hazina,
Na kijana safi leo ni kiongozi wa kesho.
Ebuyalu, Ebuyalu, taa yangu yawaka,
Ebuyalu, Ebuyalu, ndoto yangu yazuka!
Nimepata nafasi, sitaiangusha chini,
Kwa elimu na nidhamu, tutainua kijiji!
Msala si dawa, msala ni mtego,
Bangi si rafiki, ni shimo la mwanguko!
Tushike vitabu, tuache moshi wa huzuni,
Ebuyalu yetu kesho itang'aa kwa nuru!
Lakini ninapotazama nje ya lango la shule,
Naona marafiki wangu wakipambana na maisha,
Wengine walikatishwa shule na ukosefu wa karo,
Wengine wakatafuta faraja kwenye moshi wa msala.
Ee Mungu, fungua milango ya ufadhili,
Wape wenzangu nafasi, warudi kwenye elimu,
Wasije kuwa majina yaliyopotea mitaani,
Bali wawe mikono ya kuijenga Ebuyalu.
Mimi naamini, siku yetu itafika,
Tutavuka mito, tutapanda milima,
Tutakuwa walimu, madaktari, viongozi, wafanyabiashara,
Na watoto wa Ebuyalu tutairudishia heshima.
Nilipata mkono, nami nitakuwa mkono,
Nilipata nuru, nami nitawasha nuru,
Nilipata nafasi, nami sitasahau wenzangu,
Ebuyalu ikiinuka—tutainuka sote!
Ebuyalu, Ebuyalu, taa yetu yawaka,
Ebuyalu, Ebuyalu, ndoto zetu zazuka!
Alfred Amani, walimu, tunawashukuru,
Kwa kutulinda, kutuongoza, kutupa nuru!
Msala si dawa, msala ni mtego,
Bangi si rafiki, ni shimo la mwanguko!
Kalamu mkononi, matumaini moyoni,
Ebuyalu yetu kesho—itajengwa na sisi!
**Ebuyalu! — Tunasoma!
Ebuyalu! — Tunainuka!
Ebuyalu! — Hatupotei!
Ebuyalu! — Tunavuka!