Frobits
🎵 A song made on Frobits

DADA ROSE KATUPONYOKA (Remix)

Owiti Arwa Chitu · 🇰🇪 Kenya
0:000:00
Download Remix
Make your own song
Continues securely on the web
Lyrics

Chituz.
ROSE BURIANI YA KUONANA
(Dirge)
Oooooh,OOOOh,oooooh,
Lalaalallala lalala,
Iiiii,iiiii,iiii,iiiii,iiiii,
OOOOh,OOOOh,oooh,oooh
(drums beats)
Aaah Rose Anditi…
Rose… Rose......Anditi
Umekiwacha chako kiti,
Umetuacha hatusikii fiti,
Kifo tena kimetuchiti,
Machozi yanatutoka,
Mioyo yetu imevunjika,
Tusijue pa kushika,
(Slow violin for few minutes)
Rose Anditi,
Ugonjwa huu umekumaliza dada,
Ulikupa nyingi shida,
Miaka karibu mitatu,
Uvimbe wa ubongo,
Tulidhania ni uwongo,
Kama ni mkono WA mtu,ama watu....MOLA awalipie.
Kama ni mpango WA Rabuka basi atakukumbuka,
Na wanao kuwashika.
Dada Rose,Buriani ya kuonana.
Eric mume wako anabaki,
Akitazama picha yako kwa machozi,
Anajiuliza,uko wapi?”
"Hivi utarudi lini?
Jibu lake ni ukimya na huzuni.
Gloria mwanao, anamkumbuka,
Andy naye machozi yanamtoka,
Shelvin jamani bado ni mdogo,
Hana hata fahamu,
Kuwa wewe ni Marehemu,
Leo hawezi kuuliza kwa nini,
Lakini kesho atatafuta mama.
Atasema, “Mama Rose yuko wapi?”
Umemwacha shosho na kipigo Kizito,
Machozi yamemganda,
Rose Anditi,
Ugonjwa huu umekumaliza dada,
Ulikupa nyingi shida,
Miaka karibu mitatu,
Uvimbe wa ubongo,
Tulidhania ni uwongo,
Kama ni mkono WA mtu,ama watu....MOLA awalipie.
Kama ni mpango WA Rabuka basi atakukumbuka,
Na wanao kuwashika.
Dada Rose,Buriani ya kuonana.
Rafiki zako wa shule ya Msingi Nyamware, wanahangaika,
Kweli Kwa kifo chako
Wameshtuka.
Na wale WA kidato,
Shule ya Migingo Girls huko Kadiboo.
Kwa kweli wamegadhibika.
Caro rafiki yako analia,
Kweli umemtenda,
Na jinsi alikupenda,
Kumbukumbu zenu ziko moyoni,
Na machozi na majonzi, yanamshinda kuyazulia,
Caro akimtazama Shelvin anazidi kulia,
Wanajumuiya wanasema,
“Rose, pumzika kwa amani.”
Somo yako Rose Asumo na Nyamalo, Mama Sision
Mshtuko umewapata,
Matumbo yawakatakata.
Rose Anditi,
Ugonjwa huu umekumaliza dada,
Ulikupa nyingi shida,
Miaka karibu mitatu,
Uvimbe wa ubongo,
Tulidhania ni uwongo,
Kama ni mkono WA mtu,ama watu....MOLA awalipie.
Kama ni mpango WA Rabuka basi atakukumbuka,
Na wanao kuwashika.
Dada Rose,Buriani ya kuonana.
Isaya na Treezer
Kwa huzuni wanakukumbuka,
Kaka zako kina
Calvo na Ben wamebaki wakiweweseka,
Selin, Janet na Okello,
Mioyo yao imejaa simanzi na inateseka,
Monica, Atieno na Solomon, Hiki ni kitanzi cha simanzi,
Melda ameshtuka, Steve na pia Awino,
Mioyo imevunjika,
Pam kuzo walk,naye mtima wake umeteseka,
Rose Anditi,
Ugonjwa huu umekumaliza dada,
Ulikupa nyingi shida,
Miaka karibu mitatu,
Uvimbe wa ubongo,
Tulidhania ni uwongo,
Kama ni mkono WA mtu,ama watu....MOLA awalipie.
Kama ni mpango WA Rabuka basi atakukumbuka,
Na wanao kuwashika.
Dada Rose,Buriani ya kuonana.
Rose Anditi…
Eric mumeo-atakukumbuka…
Gloria mwanao mkubwa-atakukumbuka…
Andy mwanao-atakukumbuka…
Shelvin kitinda mimba-atakutafuta…
Caro rafikiyo-atakukumbuka…..
Kina Triza watakukumbuka,
Familia nzima itakukumbuka…
Kanisa la Mituri,
Fadha WA Madiany Parish,
Atakukumbuka,
Wanatufariji wote-Watakukumbuka,
Rose Anditi, lala salama…
Lala kwa amani…
Mungu akupokee katika ufalme wake…
Hadi tutakapokutana tena…
Rose Anditi,
Ugonjwa huu umekumaliza dada,
Ulikupa nyingi shida,
Miaka karibu mitatu,
Uvimbe wa ubongo,
Tulidhania ni uwongo,
Kama ni mkono WA mtu,ama watu....MOLA awalipie.
Kama ni mpango WA Rabuka basi atakukumbuka,
Na wanao kuwashika.
Dada Rose,Buriani ya kuonana.
Rose hili Kwa hakika ni pigo zito.
Rose Jaber......
Rose Nyakamware,
Rose Jahera,
Rose Nyakopere....
Rose Nyakwaya..
Rose Mwana Tufariji.

More songs by Owiti Listen to songs created by others
FROBITS