Frobits
🎵 A song made on Frobits

Agizo Kuu La Injili

Pr. Elton Mvanga · 🇹🇿 Tanzania
0:000:00
Download Remix
Make your own song
Continues securely on the web
Lyrics

(Acoustic guitar strumming with a soft fiddle melody)
(Humming)

Basi enendeni mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi
Mpendwa mwenzangu unawezaje kutulia ikiwa Bwana amekupa agizo?
Mbingu zinakuhitaji upeleke injili kwa watu wote
Unaoweza kuwafikia ulimwenguni pote.
Roho za watu zikifa pasipo kumjua Yesu Kristo utadaiwa maana Bwana amekupa agizo,
Hivyo usitulie, mavuno ni mengi sana ila watendakazi wachache,
Hebu jitokeze, chukua hatua, waambie watu Yesu anakuja.

Ondoka sasa, peleka nuru ya kweli duniani
Tumia vitabu, visambaze kama mvua ya baraka
Vitabu vitafika kule ambapo wewe huwezi kwenda
Vitabu vitasema yale ambayo midomo isingeweza kusema katika kila nyumba, kila ofisi na kila njia
Ili ulimwengu wote uone utukufu wake Bwana.

Hapo ulipo haupo kwa bahati mbaya, Mungu amekuweka
Ili uende ukazae matunda mema ambayo yatadumu
Peleka vitabu nyumba kwa nyumba, kila ofisi na mitaa
Maeneo ambayo hayajafikiwa, peleka mwanga wa uzima
Na wengine kwa mali zetu tuunge mkono kazi hii kuu
Tufadhili vitabu vya kutosha visambazwe kwa bidii
Kama miti ipukutishavyo majani wakati wa vuli
Watu wamuone Yesu maishani mwao na wadumu wakimngojea.

Ondoka sasa, peleka nuru ya kweli duniani
Tumia vitabu, visambaze kama mvua ya baraka
Vitabu vitafika kule ambapo wewe huwezi kwenda
Vitabu vitasema yale ambayo midomo isingeweza
kusema kwa kila nyumba, kila ofisi na kila njia
Ili ulimwengu wote uone utukufu wake Bwana.

Mpendwa mshiriki, kazi ya kuongoa roho ifanye agenda maishani mwako, kila kukipambazuka swali liwe nifanyaje mtu fulani amjue Yesu. Maana kuna wengi mno bado wamo gizani, wanakungoja wewe.
Usikate tamaa, panda mbegu kwa njia ya vitabu na kwa wakati wake, mbegu hizo zitamea na mwisho wa safari, taji zetu zitang'aa.

Ondoka sasa, peleka nuru ya kweli duniani
Tumia vitabu, visambaze kama mvua ya baraka
Vitabu vitafika kule ambapo wewe huwezi kwenda
Vitabu vitasema yale ambayo midomo isingeweza kusema katika, kila nyumba, kila ofisi na kila njia
Ili ulimwengu wote uone utukufu wa Bwana.

Peleka Injili nyumba kwa nyumba, kwa kila mtu,
Ulimwengu wote na umjue Yesu ni Bwana
(Fiddle solo fading out)
(Acoustic guitar closing chord)
Amina.

More songs by Pr. Listen to songs created by others
FROBITS