Eish, leo tunasherehekea!
Mama Jojo, ni siku yako, asambe!
Mama Jojo, najua leo ni siku muhimu sana
Katika maisha yako, wewe ni kipenzi changu pia ni furaha yangu
Umeongeza namba mpya katika umri wako, ni mwaka mwingine tena umeingia
Sio kwa ujanja wako, bali Mungu kakuwezesha kuifikia hii siku
Kuna wenzio walitamani tarehe kama ya leo nao washeherekee na famili zao
Ila hawapo tena katika uso wa hii dunia tena, lakini wewe kwa mapenzi ya mungu unasheherekea kipenzi changu mie
Happy birthday Mama Jojo, leo tunasherehekea kwa
Furaha, amani na upendo kwasababu ya upendo wako kwetu, pia leo tunacheza kwa shangwe kwasababu wewe ni wa kila mtu una moyo mzuri kwa kila mtu ni mcheshi kwa kila mtu kwa ndugu, marafiki na majirani pia
Kata keki kuonyesha ishara njema ya upendo kwetu sote, wote tunaimba na kucheza kwaajili ya upendo kwako
Siku yako leo ya kipekee, tunakupa sifa tele
(Yebo! Sho! Aweh!)
Wengine wako hospitalini, wanapambania afya zao
Ila wewe umebarikiwa kufika salama kabisa , ni wakati wa kufurahia na kumshukuru mungu kwa wema wake kwako
Mpigie mama hawa simu, umshukuru kwa kukuleta duniani na kukulea katika maadili mazuri ya kuwa kivutio kwa kila mtu
Pia dhidi kumwombea baba hawa aendelee kupumzika kwa amani mahala pema peponi
Alikuwa baba bora, na alikuombea na kutarajia mengi mazuri kutoka kwako ila ndiyo hivyo kazi ya mungu haina makosa kwa pamoja tunamwombea aendelee kupumzika na mungu ampunguzie adhabu ya kaburini
Happy birthday Mama Jojo, tunasherehekea
Furaha na amani, leo tunacheza
Kata keki, wote tunaimba kwa upendo
Siku yako ya kipekee, tunakupa sifa tele
(Sharp sharp! Let's go!)
Najivunia kuwa karibu yako, wewe ni fahari yangu
Pia ni wa thamani mno kwangu, Umekuwa faraja, na nuru katika maisha yangu
Tunakula, tunakunywa, na kufurahi kwa pamoja na kuonyesha
Upendo wetu kwako, tunakupenda na tunakutakia kila la kheri kipenzi chetu, dada yetu, rafiki yetu na jirani yetu
Umejawa na upendo kwa jamii yote inayokuzunguka, kwangu wewe ni lulu
Maisha yako yajae baraka, Mungu atende miujiza mikuu
Twende mbele, tusonge mbele kwa shangwe na vigelegele
Leo ni siku ya Mama Jojo, tunakupa shukrani tele
Happy birthday Mama Jojo, tunasherehekea
Furaha na amani, leo tunacheza
Kata keki, wote tunaimba kwa upendo
Siku yako ya kipekee, tunakupa sifa tele
Happy birthday kwako, Mama Jojo wangu
Furaha yako ni yangu, asambe!
(Yebo! Sharp sharp! Aweh!)
Endelea kung'aa, maisha marefu kwako.