Jamani inatuuma sana uuwiiií
Tunakulilia kaka yetu Alex Joseph Mboro
Alex Joseph Mboro, namba yako 164E
Ulikuwa mwana umoja wetu, uliyeshika nafasi
Wakiwoso tunalia, mioyo imejaa majonzi
Umeitwa na Bwana Mungu, kwenye makazi ya utukufu
Tunakumbuka ukarimu wako, tunakumbuka upendo wako
Uliwatumikia watu wako kwa moyo mweupe
Sasa umezima taa duniani, ukaenda nuruni
Yesu mpokee mtoto wetu, mpe pumziko la milele
Alex bado ulikuwa mdogo sana
Na bado tulikupenda na ulihitajika
Kwenye umoja wa Wakiwoso, kata zote sita
Nenda kaka, nenda kipenzi chetu Alex
Nenda kaka, nenda kipenzi chetu Alex
Mimi baba yako, mama yako, na ndugu zako wote
Tunakulilia sana, machozi yanatiririka mfululizo
Moyo unauma, tunatamani ungekuwa nasi bado
Lakini mapenzi ya Mungu hayahojiwi kamwe
Tunakuombea safari njema, katika njia za nuru
Kwaheri Alex, tutakukumbuka daima
Alex bado ulikuwa mdogo sana
Na bado tulikupenda na ulihitajika
Kwenye umoja wa Wakiwoso, kata zote sita
Nenda kaka, nenda kipenzi chetu Alex
Nenda kaka, nenda kipenzi chetu Alex
Wakiwoso wote tunalia juu yako Alex wetu
Wakiwoso wote tunalia juu yako Alex wetu
Mungu akupokee, upokelewe mbinguni
Na wale wote uliowasaidia hapa duniani
Mungu akupokee, upokelewe mbinguni
Na wale wote uliowasaidia hapa duniani
Uongozi mzima wa umoja wa Wakiwoso unatoa pole
Madj wote wanakuaga, kaka Alex mpendwa
Ma MC na wapambaji, tunakutakia safari njema
Chinga One nimeimba kwa upendo mdogo wangu
Tunakuaga kwa heshima, tunakuaga kwa huzuni
Kumbukumbu yako itaishi, ndani ya nyoyo zetu
Alex bado ulikuwa mdogo sana
Na bado tulikupenda na ulihitajika
Kwenye umoja wa Wakiwoso, kata zote sita
Nenda kaka, nenda kipenzi chetu Alex
Nenda kaka, nenda kipenzi chetu Alex
Nenda salama Alex Joseph Mboro
Yesu akupokee, hallelujah, ameni
Safari njema, tutaonana tena mbinguni
Glory to God, pumzika kwa amani