(Eeh Baba!)
(Halleluya!)sikia wimbo kutoka kwa stella sanga
Twende mbele zake mungu!
Mungu wetu ni mkuu, yeye ni muumba wetu!sikiliza wimbo wangu na utakubariki sana na nyimbo zangu zote zinapatikana kwa kakaangu na pacha wangu sanga studio!!nikituo pekee kinachoaminika mkoa huu wa iringa karibu sana na ubarikiwe na nyimbo zangu ameni.
Sikia habari za ajabu duniani
Namna Mungu alivyotupenda sana!Aliumba ulimwengu, akaumba sisi
Kwa mfano wake, na
Kikao mbinguni kilifanyika, Baba, Roho na Mwana
Yesu Kristo alikuwepo pale na mungu baba Akasema, "Tumfanye mwanadamu ili amiliki na kutawala"
Ooh, upendo wake hauna kifani!
Baba anatupenda, anatujali sana
Muombe bila kuchoka, yeye ni tajiri
Kila tunachohitaji, anacho mikononi
Mungu wetu yu karibu, karibu na sisi! Twende mbele zake!
Umeshuhudia mwenyewe kwenye familia
Watoto watano, mmoja anang'ara
Lakini tazama Mungu anavyofanya
Anatazama vinyonge vilivyozaraulika
Anaviinua, anaviketisha
Mahali palipoinuka, utukufu wake
Nani kama yeye? Mungu wa rehema! Mungu wetu ni mkuu.
Baba anatupenda, anatujali sana
Muombe bila kuchoka, yeye ni tajiri
Kila tunachohitaji, anacho mikononi
Mungu wetu yu karibu, karibu na sisi! Twende mbele zake!
Si kwa uwezo wetu, ni kwa neema yake
Anatuona, anatushika mkono
Asante Baba kwa upendo wako
Tunakuinua, tunakutukuza milele!
Rafiki, jamaa, jirani usikate tamaa
Baba anakuona ulipo sasa hivi
Usilie tena, mwinue Mungu juu
Yeye ni mkuu, yeye ni mlinzi
Kila goti litapigwa mbele yake
Utukufu wote ni wa Mungu wetu!
Baba anatupenda, anatujali sana
Muombe bila kuchoka, yeye ni tajiri
Kila tunachohitaji, anacho mikononi
Mungu wetu yu karibu, karibu na sisi! Twende mbele zake!
(Halleluya!)
(Asante Baba!)
Anatupenda sana, tunakuinua.
Sifa zote kwako, milele na milele.
(Ee baba!)