Frobits
🎵 A song made on Frobits

Simba Ya Mpanzu (Remix)

richardjrkassanga · 🇹🇿 Tanzania
0:000:00
Download Remix
Make your own song
Continues securely on the web
Lyrics

(Daddy happy)
(This is simba sports club)
(mama jojo, shefu omary, shefu jumanne bila kumsaha zamda hamadi )
(hii ni kwaajili ya wanasimba wote )
( Eti yanga hii unaifungajee?)
(Unaifungajee?)
Mtanii wapi mariamu mtanii

Eti yanga hii unaifungajee
Unaifungaje vipi tena mmefungwajee
mkabeni kwanza mpanzu pumbavu zenu
Simba ya Mpanzu unaizuiajee
wapi kasura mpe salama mama jifiti mwambie
Hapa Mpanzu pale Oura kule Libase
mabeki zake wamkabe nani maana sio boka wala baka hawawezi kuwakaba hao mabwana
Huyo Chilambo hajulikani anachezaje
Beki au kiungo ama mshambuliaji mcheze
Nyuma yupo katikati unamkuta
Kabla ya kumzuia kashafika mbele ya box
la wapinzani anatoa pasi kwa mpanzu kabla ya kufika kwa mpanzu pasi inaelekezwa kwa
Chama hapo nenda taratibu maana unaweza pata aibu ya mwaka
Ukimfuata hovyo utaambulia tobo
Utadhalilishwa sana na unaweza vunjika nyonga bure
Kagoma amegoma kweli kupitwa kizembe
Naona pira biriani limerudi wapinzani wanatafutana hapa.

Eti yanga hii unaifungajee
yangaa hii unaifungajee
Vipi leo mmefungwajee jiulizeni
Simba ya Mpanzu unaizuiajee
Unaizuiajee
Hii ndio Simba tunayoijua simba ya asali na tende
Kwa huu moto hatushikiki wa hatubabaishwi hawa vyura wa jangwani
Eti yanga hii unaifungajee
unaifungajee haya sasaa
Simba ya Mpanzu unaizuiajee
Huyo Mpanzu unamzuiajee.

Toure askari wa doria muda wote
Yuko bize kuangalia maadui wanapita wapi
Hapa unakutana na beki mtanashati
Sura ya upole matendo ya kikatili
Anaitwa Rushain anakaba na kutoa pasi
Anamgusia Neo Maema kwa ustadi
Maema anampa Jabari pasi elekezi kabisa
Jabari anasogea anaitanguliza mbele kidogo
Anaitanguliza kwa Libase speed mashine
Libase anatanua uwanja anaimwaga kati
Inamkuta Chama kwake Mpanzuuuuu
Goooo.... Hii ni simba braza weka mbali hawa utopolo
Mchezo wa soka unahitaji akili nyingi
Sio kupiga kelele bila kuwa na mbinu.
Pumzika kwa amani mzee mpili

Eti yanga hii unaifungajee
unaifungajee
Simba ya Mpanzu unaizuiajee
unaizuiajee
Hii ndio Simba weka mbali na utopolo
Sisi ni moto hatushikiki wala hatuchekeshi
Eti yanga hii unaifungajee
Unaifungaje kweli unaifungajee
Simba ya Mpanzu unaizuiajee
unaizuiajee.

Tunacheza soka safi tunapiga pasi za kutosha
tunakubonda huku tuna kupapasa
Wapinzani wanahaha wanashindwa kuzuia
Simba ya Mpanzu ni balaa mtaani
Ona pasi za kifuani ona pasi za miguu
Soka ni sanaa soka ni burudani
Simba imetulia Simba inafurahisha
Utopolo wameishiwa hawana la kusema.

Kila kona ya uwanja ni shughuli pevu
Maema anadhibiti eneo la kati
Chama anapanga mipango ya ushindi
Mpanzu anamalizia kazi kwa ustadi
Ni mwendo wa goli mpaka mwisho wa mechi
Watazamaji wanashangilia kwa nguvu
Hii ndio Simba ya kimataifa bwana
Hamuwezi kutuzuia hata kwa dawa
Endeleeni kuota sisi tuko kileleni
Simba nguvu moja ubaya ubwela season 3.

Eti yanga hii unaifungajee
Unaifungaje kweli unaifungajee
Simba ya Mpanzu unaizuiajee
unaizuiajee
Hii ni Simba braza usiifananishe gongo wazi
Sisi ni moto wa kuotea mbali hatushikiki wala hatuchekeshi
Eti yanga hii unaifungajee
Vipi leo mmefungwajee
Simba ya Mpanzu unaizuiajee
unaizuiajee.

(Simba ya Mpanzu)
(Weka mbali)
(Mambo ya utopolo tuyaache)
(Sisi tunacheza soka)
(Haya haya haya)
(Simba damu damu!)
(Tunaenda zetu kileleni)
(Mpanzu ndani ya nyumba!)
(Soka safi soka burudani)
(Salute!)
Hii ni kwaajili yetu sote wanamsimbazi daddy happy, mama jojo, shefu omary, shefu jumanne na zamda hamadi
Mariamu mtani karibu msimbazi huko nyuma mwiko kutakuuwa bure mke wangu...
mimi ni simbaaaaaa

More songs by richardjrkassanga Listen to songs created by others
FROBITS