Naiombea Tanzania, nchi yangu nzuri
Tunainua sauti zetu kwako Mungu
Kabla ya yote twaomba, dua na sala na maombezi
Kwa ajili ya watu wote, katika kila pembe ya nchi
Kwa wafalme na wote wenye mamlaka, tuishi kwa utulivu
Katika utauwa na ustahivu, maisha ya amani tele
Asante Yesu, kweli ni vyema mbele zako
Ulitaka wote waokolewe, na kujua kweli yako
Ee Mungu ibariki Tanzania, sikia toka mbinguni
Kama watu wako tunajinyenyekesha, na kuomba kwako
Uiponye nchi yetu, na kusamehe dhambi zetu
Tunautafuta uso wako, kwa ajili ya taifa hili
Tunainua viongozi wetu, mikononi mwako Bwana
Hallelujah, sifa na utukufu ni vyako
Namuombea Rais wetu, na Makamu wa Rais
Na Waziri Mkuu pia, Baraza la Mawaziri wote
Spika wetu na Wabunge, hekima iwe juu yao
Wakuu wa Mikoa na Wilaya, wafanye kazi kwa uaminifu
Afisa tarafa, watendaji wa kata na vijiji pia
Uweongoze hatua zao, katika haki na kweli
Yesu Bwana, tunakuamini wewe pekee
Ee Mungu ibariki Tanzania, sikia toka mbinguni
Kama watu wako wakijinyenyekesha, na kuomba kwako
Utaponya nchi yetu, na kusamehe dhambi zetu
Naitafuta uso wako, kwa ajili ya taifa hili
Tunainua viongozi wetu, mikononi mwako Bwana
Asante Yesu, sifa na utukufu ni vyako
Wizara zote za Elimu, Afya na Maendeleo
Miundombinu na usafiri, Ulinzi na Usalama wetu
Idara zote za serikali, mashirika ya umma na dini
Zote ziko mikononi mwako, uwe mlinzi wa taifa
Utupe neema, utupe umoja, utupe nuru yako
Praise Him, utupe ulinzi wako milele
Tunakataa migogoro, tunakaribisha upendo
Kila ofisi iwe mahali, pa kutumikia wananchi
Bariki kila mkono, unaojenga Tanzania yetu
Uwe mwamba wetu, uwe kimbilio letu daima
Yesu uwe mfalme, juu ya kila uamuzi
Amen, twakuamini wewe ni mwema
Ee Mungu ibariki Tanzania, sikia toka mbinguni
Kama watu wako wakijinyenyekesha, na kuomba kwako
Utaponya nchi yetu, na kusamehe dhambi zetu
Naitafuta uso wako, kwa ajili ya taifa hili
Tunainua viongozi wetu, mikononi mwako Bwana
Glory, sifa na utukufu ni vyako
Ibariki Tanzania, tunakuomba Bwana
Ibariki Tanzania, tunakutumainia wewe
Yesu ndiye tumaini letu, kwa taifa hili
Amen, amen, tunazidi kukuamini
Utatenda makuu, kwa ajili ya Tanzania